EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili

Dinah Sungu Osango, Mwenda Mbatiah, Rayya Timammy

Journal of Kiswahili and Other African Languages · 2024

DOI: 10.58721/jkal.v2i1.410 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2024. Verfasst von Dinah Sungu Osango und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala haya yanachunguza ngazi ya utambuzi na uamilifu wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa makusudi kwa uchunguzi huu. Riwaya hizo ni; Nyuso za Mwanamke (S. Mohamed, 2010), Harufu ya Mapera (K. Wamitila, 2012), Hujafa Hujaumbika (F. Kagwa, 2018), Haini (A. Shafi, 2002), na Ndoto ya Almasi (K. Walibora, 2006). Ngazi ya utambuzi ni mojawapo ya ngazi mbalimbali za ufokasi zilizopendekezwa na wananaratolojia. Kimsingi, ufokasi ni mtazamo ambao huchukuliwa katika kuwasilisha simulizi na kuikuza hadithi kwa ujumla. Data ya kuudhibiti na kuthibitisha madai ya mjadala wetu imetolewa katika riwaya teule. Uteuzi wa riwaya hizi unahalalishwa kwa misingi kwamba, hizi ni riwaya zilizo na matini pana zinazowezesha udondoaji wa mifano faafu inayodhihirisha ngazi za ufokasi na wakati huo huo kudhihirisha uamilifu wa ngazi hizo katika simulizi. Mjadala wa kimsingi katika makala haya umekitwa na kuongozwa na madai ya teneti za kimsingi za nadharia ya naratolojia ambayo inatambua ufokasi na uhusika kama vipengele muhimu katika uwasilishaji wa simulizi.

Zitieren

APA

Osango, D. S., Mbatiah, M., & Timammy, R. (2024). Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages. https://doi.org/10.58721/jkal.v2i1.410

Vancouver

Osango DS, Mbatiah M, Timammy R. Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages. 2024. doi:10.58721/jkal.v2i1.410

BibTeX
@article{Osango2024,
  author = {Osango, Dinah Sungu and Mbatiah, Mwenda and Timammy, Rayya},
  title = {Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili},
  journal = {Journal of Kiswahili and Other African Languages},
  year = {2024},
  doi = {10.58721/jkal.v2i1.410}
}
Kostenlos starten →