EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Mabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018

Pamela Anyango, Edwin Masinde, Jessee Murithi

East African Journal of Swahili Studies · 19.11.2026 · 9 (3) · 500-515

DOI: 10.37284/jammk.9.3.6328 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 19.11.2026. Verfasst von Pamela Anyango und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Riwaya za kipelelezi zimefanyiwa uchanganuzi huku uzingativu mwingi ukiwekwa kwenye kipengele cha uforensiki, mtindo na ploti (taz. Kamau, 1992, Ngugi, 2016 na Kombo, 2018). Tafiti hizi za awali zimedhihirisha kuchunguza kipengele kimoja kwa upekee bila kuzingatia uwiano wa vipengele vyenyewe katika riwaya za kipelelezi. Hili lilichochea kuwepo kwa haja ya kuchunguza utangamano wa vipengele vya kimuundo na mabadiliko yake katika riwaya teule za Kiswahili za kutoka mwaka wa 1957-2018. Utafiti basi umechanganua mabadiliko na maendeleo ya vipengele vya kimuundo katika riwaya teule za kipelelezi za Kiswahili za kutoka mwaka wa 1957-2018 (za karne ya 20 na za karne ya 21). Riwaya zilizoteuliwa katika utafiti huu ni za kutoka mwaka wa 1957 hadi wa 2000 (za karne ya 20) Mizimu ya Watu wa Kale (Abdalla, 1957), Simu ya Kifo (Katalambula, 1965), Mpelelezi na Genge la Wezi (Levi, 1975) na zile za kutoka mwaka wa 2001 hadi wa 2018 (za karne ya 21). Mkononi mwa Nunda (Mtobwa, 2011), Msako 1 (Sudi, 2016) na Msako 2 (Sudi, 2016). Riwaya hizi ziliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia kipengele cha muundo na wakati. Katika makala hii, muundo ulichunguzwa kwa undani kwa kuzingatia vipengele vya muundo ambavyo ni wahusika, maudhui na ploti. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa na Ferdinand De Saussure (1906) katika tawi la isimu. Baadaye, nadharia hii ilitumika na Vladimir Propp (1928) na kuendelezwa na Levi-Strauss (1963) aliyeibuka na wazo kwamba Umuundo unaweza kutumika kuchanganua sayansi za kijamii ikiwemo fasihi. Kuna waitifaki wa hivi karibuni kama vile Stanton (2007) ambaye anaegemea zaidi tawi la kifasihi. Mhimili mkuu uliotuongoza ni kuwa, vipengele vya kimuundo; wahusika, maudhui na ploti huchangiana na kukamilishana. Aidha, wazo la Jakobson (1960) kuwa lugha ya kifasihi hukua na kubadilika kulingana na mabadiliko ya kijamii, kitamaduni na ya kiteknolojia lilituongoza katika kuchunguza mabadiliko na maendeleo ya muundo wa riwaya teule za kipelelezi. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba ambapo mtafiti alisoma riwaya teule, makala, vitabu na kusakura mtandao ili kukusanya data inayofaa na kupata uelewa mpana wa mada. Matokeo yalionyesha kwamba, ingawa kuna ufomyula katika muundo wa riwaya za kipelelezi, kuna mabadiliko yanayodhihirika kiwakati. Riwaya za kutoka mwaka wa 2000-2018 (za karne ya 21) zimeonyesha mabadiliko kutoka kwa zile za kutoka mwaka wa 1957-2000 (za karne ya 20) katika misingi ya vipengele vya muundo ambavyo ni: usawiri wa mhusika mpelelezi mkuu, mhusika mkinzani na wa kike, mabadiliko ya kimaudhui, kiploti, kiteknolojia na kimandhari.

Zitieren

APA

Anyango, P., Masinde, E., & Murithi, J. (2026). Mabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 500-515. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6328

Vancouver

Anyango P, Masinde E, Murithi J. Mabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):500-515. doi:10.37284/jammk.9.3.6328

BibTeX
@article{Anyango2026,
  author = {Anyango, Pamela and Masinde, Edwin and Murithi, Jessee},
  title = {Mabadiliko katika Muundo na Maumbo katika Riwaya Teule za Kipelelezi za Kiswahili: 1957-2018},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {3},
  pages = {500--515},
  doi = {10.37284/jammk.9.3.6328}
}
Kostenlos starten →