EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Masuala ya Ekolojia katika Bunilizi Teule za Fasihi ya Watoto ya Kiswahili Ikisiri

Martin Karani Ndeke, Shadrack Kirimi, Mary Kanyua

Editon Consortium Journal of Kiswahili · 16.11.2026 · 7 (1) · 177-187

DOI: 10.51317/fg87dq15 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Editon Consortium Journal of Kiswahili, online erschienen am 16.11.2026. Verfasst von Martin Karani Ndeke und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala hii inalenga kuchunguza mchango wa fasihi ya watoto ya Kiswahili katika kukuza uelewa wa kiekolojia kwa kuchanganua bunilizi teule za Fisi Mtunza Miti (Kobia, 2008), Sifuri Nyani Mtalii (Matundura, 2017) na Kijiji cha Ukame (Babusa, 2020). Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia ya Glotfelty na Fromm (1996). Data zilikusanywa kwa kutumia mbinu ya usomaji makinifu na kuchambuliwa kwa kutumia uchambuzi wa matini. Utafiti ulitumia muundo wa kimaelezo na mbinu ya utafiti wa kimaktaba, huku data zikiwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Matokeo yalibainisha kuwa bunilizi teule zimeangazia vyanzo vya mabadiliko ya tabianchi, athari zake na mikakati ya kukabiliana nazo. Vyanzo vilivyojitokeza ni pamoja na uzalishaji wa makaa na ukataji wa miti, huku athari zikihusisha ukame, ongezeko la joto duniani, uhaba wa chakula na vifo vya viumbe hai. Aidha, bunilizi hizo zimesisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira kama wajibu serikali na wa kila mwanajamii. Makala hii inahitimisha kuwa fasihi ya watoto ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ya kujenga mwamko na uwajibikaji wa kimazingira miongoni mwa watoto. Hivyo, inapendekezwa kuwa waandishi wajumuishe maudhui ya kiekolojia katika kazi zao, walimu watumie bunilizi hizo kama nyenzo za kufundishia na wadau wa elimu waimarishe ujumuishaji wa masuala ya mazingira katika mitaala. Utafiti huu una umuhimu katika kuonesha nafasi ya fasihi ya watoto ya Kiswahili katika kuelimisha jamii kuhusu changamoto za kimazingira na kuhamasisha utunzaji endelevu wa mazingira.

Zitieren

APA

Ndeke, M. K., Kirimi, S., & Kanyua, M. (2026). Masuala ya Ekolojia katika Bunilizi Teule za Fasihi ya Watoto ya Kiswahili Ikisiri. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 7(1), 177-187. https://doi.org/10.51317/fg87dq15

Vancouver

Ndeke MK, Kirimi S, Kanyua M. Masuala ya Ekolojia katika Bunilizi Teule za Fasihi ya Watoto ya Kiswahili Ikisiri. Editon Consortium Journal of Kiswahili. 2026;7(1):177-187. doi:10.51317/fg87dq15

BibTeX
@article{Ndeke2026,
  author = {Ndeke, Martin Karani and Kirimi, Shadrack and Kanyua, Mary},
  title = {Masuala ya Ekolojia katika Bunilizi Teule za Fasihi ya Watoto ya Kiswahili Ikisiri},
  journal = {Editon Consortium Journal of Kiswahili},
  year = {2026},
  volume = {7},
  number = {1},
  pages = {177--187},
  doi = {10.51317/fg87dq15}
}
Kostenlos starten →