EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Mbinu za Lugha Zinazotumiwa katika Matangazo ya Biashara ya Kampuni ya Safaricom.

Jane Kanini Maithya, Prof. Nabea Wendo, Prof. James Ogola Onyango

Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK) · 2022

DOI: 10.51317/eajk.v2i1.104 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 2022. Verfasst von Jane Kanini Maithya und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Matangazo ya biashara hunuiwa kuwajuvya wateja kuhusu kuwepo kwa bidhaa za kampuni mbalimbali na kuwahimiza wanunue bidhaa hizo. Vahid na Esmae’li(2012) wanasema kuwa licha ya kutimiza lengo hilo,matangazo hayo vilevile hunuiwa kuchekesha, kupotosha au kuwadanganya wateja ili wavutiwe na bidhaa inayotangazwa. Hayo hutekelezwa kupitia kwa lugha inayotumiwa. Waundaji huteua mbinu za lugha zilizo na uwezo wa kuwafanya wateja watamani kununua bidhaa hata ikiwa hawazihitaji. Utafiti huu unachunguza mbinu za lugha zinazotumiwa katika matangazo ya biashara ya Kampuni ya Safaricom. Ni kampuni maarufu ya mawasiliano nchini Kenya inayotoa huduma mbalimbali za mawasiliano kama vile uuzaji wa aina mbalimbali za rununu, huduma za intaneti, M-pesa, M-shwari na kadhalika.Kampuni hiyo hutumia mbinu mbalimbali za lugha zinazoundwa kwa ubunifu mwingi kwa nia ya kuvuta nadhari ya wateja wake. Ingawa kuna tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu Kampuni ya Safaricom, hakuna utafiti umechunguza na kuzieleza mbinu hizo kwa kina, pengo ambalo limezibwa na utafiti huu. Data katika makala haya ilipatikana kutoka kwa mtandao wa intaneti ambapo mtafiti alipakua matangazo ya Safaricom aina ya picha na video. Alizitumia kutoa mifano ya mbinu mbalimbali zinazotumiwa kwenye kwenye matangazo hayo. Utafiti ulibainisha kuwa waundaji wa matangazo ya Safaricom hutumia mbinu mbalimbali za lugha zinazoundwa kwa ubunifu wa hali ya juu kwa nia ya kuwajuvya wateja kuhusu kuwepo kwa bidhaa na huduma zao na vilevile kuwavutia wazinunue.

Zitieren

APA

Maithya, J. K., Wendo, P. N., & Onyango, P. J. O. (2022). Mbinu za Lugha Zinazotumiwa katika Matangazo ya Biashara ya Kampuni ya Safaricom. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). https://doi.org/10.51317/eajk.v2i1.104

Vancouver

Maithya JK, Wendo PN, Onyango PJO. Mbinu za Lugha Zinazotumiwa katika Matangazo ya Biashara ya Kampuni ya Safaricom. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). 2022. doi:10.51317/eajk.v2i1.104

BibTeX
@article{Maithya2022,
  author = {Maithya, Jane Kanini and Wendo, Prof. Nabea and Onyango, Prof. James Ogola},
  title = {Mbinu za Lugha Zinazotumiwa katika Matangazo ya Biashara ya Kampuni ya Safaricom},
  journal = {Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)},
  year = {2022},
  doi = {10.51317/eajk.v2i1.104}
}
Kostenlos starten →