Athari za Kimofolojia za Lugha ya Kihehe katika Ujifunzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Mkoa wa Iringa
East African Journal of Swahili Studies · 08.08.2026 · 9 (2) · 181-201
DOI: 10.37284/jammk.9.2.5514 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 08.08.2026. Verfasst von Elizabeth Itaja. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Utafiti huu umechunguza athari za kimofolojia za lugha ya Kihehe katika ujifunzaji wa Kiswahili kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoani Iringa, hususani Wilaya ya Kilolo. Lengo kuu lilikuwa kubainisha namna vipengele vya kimofolojia vya Kihehe vinavyoathiri matumizi ya Kiswahili kama lugha ya pili kwa wanafunzi. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Uhawilishaji Lugha ya Lado (1957), inayosisitiza kuwa lugha ya kwanza huweza kuathiri ujifunzaji wa lugha ya pili kwa kuhamisha vipengele vya kifonolojia, kimofolojia na kisarufi. Utafiti ulitumia mkabala wa kimaelezo, na data zilikusanywa kwa kutumia ushuhudiaji na mahojiano. Sampuli ilihusisha washiriki 76, wakiwemo wanafunzi 60 na walimu 16 wa Kiswahili kutoka shule nne za msingi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa wanafunzi huathiriwa na Kihehe katika matumizi ya Kiswahili, hali inayosababisha makosa ya kimofolojia na kimofofonolojia. Athari hizo zimejitokeza katika matumizi ya viambishi vya nafsi, uchopekaji wa fonimu na irabu, ubadilishaji wa sauti, pamoja na makosa katika maumbo ya udogoshi na ukubwa. Kwa ujumla, utafiti umebaini kuwa makosa haya hutokea kwa kufuata kanuni za Kihehe, na hivyo kuthibitisha kuwa lugha ya kwanza ina mchango mkubwa katika ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya pili. Utafiti unapendekeza matumizi ya mbinu shirikishi na tendaji katika ufundishaji wa Kiswahili, mafunzo endelevu kwa walimu, na kuzingatia muktadha wa lugha mama katika mitaala ili kupunguza athari hasi za Kihehe katika ujifunzaji wa Kiswahili
Zitieren
APA
Itaja, E. (2026). Athari za Kimofolojia za Lugha ya Kihehe katika Ujifunzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Mkoa wa Iringa. East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 181-201. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5514
Vancouver
Itaja E. Athari za Kimofolojia za Lugha ya Kihehe katika Ujifunzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Mkoa wa Iringa. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):181-201. doi:10.37284/jammk.9.2.5514
BibTeX
@article{Itaja2026,
author = {Itaja, Elizabeth},
title = {Athari za Kimofolojia za Lugha ya Kihehe katika Ujifunzaji wa Kiswahili kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Mkoa wa Iringa},
journal = {East African Journal of Swahili Studies},
year = {2026},
volume = {9},
number = {2},
pages = {181--201},
doi = {10.37284/jammk.9.2.5514}
}
EUVIMED