Muundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018
East African Journal of Swahili Studies · 19.11.2026 · 9 (3) · 561-579
DOI: 10.37284/jammk.9.3.6327 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 19.11.2026. Verfasst von Pamela Anyango und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Makala hii inalenga kuchanganua muundo na maumbo tangamano ya riwaya teule za kipelelezi za Kiswahili za kutoka 1957-2018. Tafiti za awali (kama vile utafiti wa Ngugi, 2016) zimedhirihisha kuchunguza kipengele kimoja kwa upekee bila kuzingatia uwiano wa vipengele vyenyewe katika riwaya za kipelelezi. Hili lilichochea kuwepo kwa haja ya kuchunguza utangamano wa muundo na maumbo katika riwaya teule kutoka 1957-2018. Katika kazi hii, muundo ulichunguzwa kwa undani kwa kuzingatia vipengele vya muundo kama vile: wahusika, maudhui, ploti, na mandhari. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Umuundo iliyoasisiwa Ferdinand De Saussure (1906) katika tawi la isimu. Baadaye, nadharia hii ilitumika na Propp (1928) na kuendelezwa na Levi-Strauss (1946) aliyeibuka na wazo kwamba nadharia hii inaweza kutumika kuchanganua sayansi za kijamii ikiwemo fasihi. Kuna waitifaki wa hivi karibuni kama vile Barthes (1977), Culler (1975), Scholes na Stanton (2007) ambaye anaegemea zaidi tawi la kifasihi. Stanton (2007) anaamini kwamba nadharia ya umuundo ni muhimu sana katika kuhakiki riwaya. Mhimili mkuu uliotuongoza ni kuwa vipengele vya kimuundo; wahusika, maudhui. Ploti na mandhari huchangiana na kukamilishana. Aidha, wana umuundo waliamini kuwa sheria ya umuundo hushughulikia zaidi muingiliano bali siyo utengano. Utafiti huu ulikuwa wa kimaktaba ambapo mtafiti alijukumika kusoma riwaya teule ili kupata data ya kimsingi. Data ya upili ilipatikana kwa kusoma makala na vitabu. Aidha, sampuli iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ambapo riwaya teule ziliteuliwa kimaksudi kwa kuzingatia kipengele cha muundo na wakati, yaani zile zilizoandikwa karne ya 19 na zile za karne ya 20. Riwaya zilizoteuliwa katika utafiti huu za kutoka mwaka wa 1957 hadi wa 2000 (za karne ya 20) Mizimu ya Watu wa Kale (Abdalla, 1957), Simu ya Kifo (Katalambula, 1965), Mpelelezi na Genge la Wezi (Levi, 1975) na zile za kutoka mwaka wa 2001 hadi wa 2018 (za karne ya 21) Mkononi mwa Nunda (Mtobwa, 2011), Msako 1 (Sudi, 2016) na Msako 2 (Sudi, 2016). Riwaya hizi ziliteuliwa kwa kuwa za karne ya 20 zina data hitajika ya vipengele vya kimuundo vilevile za karne ya 21 zinaonyesha utangamano wa kimuuundo na vile vya karne ya 20. Matokeo yalionyesha kuwa riwaya za kipelelezi za Kiswahili zilizoandikwa kutoka mwaka wa 1957-2018 zilisawiri utangamano kwa kiwango kikubwa katika vipengele vyote vya kimuundo. Kama riwaya zingine za kipelelezi, ufomyula unadhihirika katika vipengele vyote vya kimuundo ambavyo ni wahusika, ploti maudhui na mandhari. Kwa mfano kuna jukumu la mpelelezi maalum, kama mhusika mkuu mwenye sifa bainifu, linalojitokeza katika riwaya zote sita. Fauka ya hayo, miisho ya riwaya zote teule zilidhihirisha urejesho wa utulivu; Wema kushinda uovu
Zitieren
APA
Anyango, P., Masinde, E., & Murithi, J. (2026). Muundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 561-579. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6327
Vancouver
Anyango P, Masinde E, Murithi J. Muundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):561-579. doi:10.37284/jammk.9.3.6327
BibTeX
@article{Anyango2026,
author = {Anyango, Pamela and Masinde, Edwin and Murithi, Jessee},
title = {Muundo na Maumbo Tangamano katika Riwaya za Kipelelezi za Kiswahili: 1957—2018},
journal = {East African Journal of Swahili Studies},
year = {2026},
volume = {9},
number = {3},
pages = {561--579},
doi = {10.37284/jammk.9.3.6327}
}
EUVIMED