EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Jinsi Wahusika Wanavyochangia Katika Mabadiliko ya Tabianchi Katika Tamthilia za Shimo katika Anga (2022) na Majira ya Utasa (2015)

Wafula Ann Sophy, Edwin Masinde

East African Journal of Swahili Studies · 07.07.2026 · 9 (2) · 1-12

DOI: 10.37284/jammk.9.2.5290 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 07.07.2026. Verfasst von Wafula Ann Sophy und 1 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala hii imeonyesha jinsi wahusika mbalimbali katika tamthilia za Shimo katika Anga (2022) na Majira ya Utasa (2015) wanavyochangia katika mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni suala ibuka ambalo limeathiri ulimwengu mzima na chanzo chake kuu ni shughuli za binadamu (Sangili, 2015). Waandishi wa tamthilia teule wameonyesha michango ya wahusika kupitia kwa semi zao, tabia na maamuzi yao katika mazingira. Watafiti mbalimbali wameshughulikia suala la nafasi ya wahusika na kuhusisha na mazingira kwa kuegemea mikabala tofautitofauti. Sabula (2014) ameshughulikia nafasi ya ufeministi wa kiekolojia katika fasihi katika riwaya ya Nakuruto. Naye Momanyi (2025) amechunguza mchango wa fasihi katika uhifadhi wa mazingira. Kutokana na uchunguzi wa watafiti hawa, imebainika kuwa tafiti za awali kuhusu nafasi za wahusika na kazi za kifasihi zimejikita kwenye mchango wa jinsia mahsusi katika uhifadhi wa mazingira na jinsi fasihi kwa jumla huchangia katika uhifadhi wa mazingira. Kwa hivyo, pana haja ya kuchunguza jinsi wahusika mbalimbali wanachangia katika mabadiliko ya tabianchi kwa kurejelea tamthilia teule. Makala hii imeongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Kiekolojia ambayo iliwekewa msingi na William Ruekert (1978) kisha ikaendelezwa na Glotferty na Fromm (1996). Uhakiki wa Kiekolojia unahusika na kuchambua kazi za fasihi kwa kuangalia masuala ya kiekolojia yanavyotagusana na binadamu kwa njia chanya au hasi. Nguzo hii ndiyo iliyotumika katika utafiti huu kwa vile inafafanua namna wahusika katika tamthiwlia teule wanaingiliana na mazingira wanamoishi na kusababisha mabadiliko ya tabianchi. Data iliyotumika ilitolewa maktabani, ambapo tamthilia teule na makala inayohusiana na mada ilisomwa na kuchambuliwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo ya utafiti umetekelezwa kwa njia ya maelezo kwa kuambatanishwa na kauli za wahusika. Matokeo ya utafiti yameonyesha kuwa katika tamthilia teule, wahusika mbalimbali wamechangia katika mabadiliko ya tabianchi.

Zitieren

APA

Sophy, W. A., & Masinde, E. (2026). Jinsi Wahusika Wanavyochangia Katika Mabadiliko ya Tabianchi Katika Tamthilia za Shimo katika Anga (2022) na Majira ya Utasa (2015). East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 1-12. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5290

Vancouver

Sophy WA, Masinde E. Jinsi Wahusika Wanavyochangia Katika Mabadiliko ya Tabianchi Katika Tamthilia za Shimo katika Anga (2022) na Majira ya Utasa (2015). East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):1-12. doi:10.37284/jammk.9.2.5290

BibTeX
@article{Sophy2026,
  author = {Sophy, Wafula Ann and Masinde, Edwin},
  title = {Jinsi Wahusika Wanavyochangia Katika Mabadiliko ya Tabianchi Katika Tamthilia za Shimo katika Anga (2022) na Majira ya Utasa (2015)},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {2},
  pages = {1--12},
  doi = {10.37284/jammk.9.2.5290}
}
Kostenlos starten →