EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Kubainisha Sifa za Wahusika Walemavu katika Kipindi cha Sultana kwenye Runinga ya Citizen

Caroline Kemunto Getate, Richard Makhanu Wafula

East African Journal of Swahili Studies · 08.08.2026 · 9 (2) · 202-213

DOI: 10.37284/jammk.9.2.5517 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 08.08.2026. Verfasst von Caroline Kemunto Getate und 1 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Utafiti huu ulilenga kubainisha sifa za wahusika walemavu katika kipindi cha Sultana kilichopeperushwa kwenye runinga ya Citizen nchini Kenya kuanzia Machi 2022 hadi Julai 2023. Tafiti nyingi za awali zimejikita katika usawiri wa wahusika walemavu katika fasihi na vyombo vya habari, huku nyingi zikionyesha taswira hasi za wahusika hao. Utafiti huu ulilenga kuchunguza sifa zinazodhihirishwa na wahusika walemavu katika kipindi hicho ili kuelewa namna wanavyosawiriwa katika jamii kupitia runinga. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Maigizo ya Turner (1969) inayosisitiza umuhimu wa kuakisi maisha halisi ya jamii kupitia vitendo vya waigizaji. Utafiti ulifanywa maktabani na nyanjani. Data ilikusanywa kwa kutazama na kuchanganua vipindi vya Sultana pamoja na kufanya mahojiano na wahusika walemavu waliohusika katika kipindi hicho. Sampuli iliteuliwa kimaksudi ili kupata washiriki waliokuwa na taarifa muhimu kuhusu suala lililochunguzwa. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa njia ya maelezo kwa kuzingatia lengo la utafiti na mihimili ya nadharia iliyotumika. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa wahusika walemavu katika kipindi cha Sultana wanadhihirisha sifa mbalimbali. Wahusika walemavu wa viungo walionekana kuwa na sifa za ukakamavu, uvumilivu, hekima, hasira, ubinafsi na upweke. Kwa upande mwingine, wahusika walemavu wa tabia walidhihirisha sifa za tamaa, ukatili, udanganyifu, ukaidi, uchochezi na taasubi ya kiume. Utafiti ulihitimisha kuwa kipindi cha Sultana kinawasawiri wahusika walemavu kwa namna inayodhihirisha sifa mbalimbali chanya na hasi zinazopatikana pia kwa wanajamii wengine. Utafiti huu unachangia maarifa kuhusu usawiri wa wahusika walemavu katika vipindi vya televisheni vya Kiswahili nchini Kenya.

Zitieren

APA

Getate, C. K., & Wafula, R. M. (2026). Kubainisha Sifa za Wahusika Walemavu katika Kipindi cha Sultana kwenye Runinga ya Citizen. East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 202-213. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5517

Vancouver

Getate CK, Wafula RM. Kubainisha Sifa za Wahusika Walemavu katika Kipindi cha Sultana kwenye Runinga ya Citizen. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):202-213. doi:10.37284/jammk.9.2.5517

BibTeX
@article{Getate2026,
  author = {Getate, Caroline Kemunto and Wafula, Richard Makhanu},
  title = {Kubainisha Sifa za Wahusika Walemavu katika Kipindi cha Sultana kwenye Runinga ya Citizen},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {2},
  pages = {202--213},
  doi = {10.37284/jammk.9.2.5517}
}
Kostenlos starten →