EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili

Hadija Jilala

Journal of Kiswahili and Other African Languages · 2024

DOI: 10.58721/jkal.v2i2.518 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2024. Verfasst von Hadija Jilala. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Dhana ya akili unde au akili bandia inarejelea mwigo au ukadiriaji wa akili ya binadamu katika mashine. Lengo la akili unde ni pamoja na matumizi ya kompyuta yaliyoboreshwa kuhoji na kutambua mambo anuwai unde na ya tasnia mbalimbali (Jurafsky na Martin, 2020). Makala hii inalenga kutathmini matumizi ya akili unde kama nyenzo ya kutafsiri matini za Kiingereza kwenda Kiswahili. Data ya makala hii imekusanywa maktabani kwa kupitia maandiko na pia uwandani kwa kuwahoji wanataaluma mbalimbali. Uchambuzi na uwasilishaji wa data ya makala hii umeongozwa na Mkabala wa Uchambuzi wa Maudhui ya Krippendorff (2004). Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa akili unde ina ubora kwa vile hufanya kazi kwa kasi, gharama ni nafuu, urahisi, kutafsiri lugha nyingi na unyumbufu wa kuunganishwa na teknolojia nyingine. Kwa upande mwingine makala hii imebainisha udhaifu wa matumizi ya akili unde kama vile kutozingatia muktadha, kukosa ubunifu, tofauti za kiisimu, kukosa usalama na upinzani wa wanaisimu. Kutokana na udhaifu huo, Makala hii inapendekeza kuwa uwekwe uangalizi wa binadamu katika mifumo, kushughulikia utata, kuboresha mifumo kila muda, kuwekwe sehemu ya maoni ya mtumiaji na matumizi ya mbinu msetu. Hivyo, ni muhimu kuweka usawa kati ya ufanisi wa mashine na uelewa wa watafsiri wa kibinadamu katika uendelezaji na utekelezaji wa akili unde katika tafsiri.

Zitieren

APA

Jilala, H. (2024). Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages. https://doi.org/10.58721/jkal.v2i2.518

Vancouver

Jilala H. Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili. Journal of Kiswahili and Other African Languages. 2024. doi:10.58721/jkal.v2i2.518

BibTeX
@article{Jilala2024,
  author = {Jilala, Hadija},
  title = {Tathmini ya Matumizi ya Akili Unde Kama Nyenzo ya Kutafsiri Matini za Kiingereza Kwenda Kiswahili},
  journal = {Journal of Kiswahili and Other African Languages},
  year = {2024},
  doi = {10.58721/jkal.v2i2.518}
}
Kostenlos starten →