EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Taswira ya Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu wa Karne ya 21: Uchambuzi wa Shairi la Mahavule na Jamii

Sumaiya Yunus Mwamzandi, Mosol Kandagor, Magdaline Wafula

Editon Consortium Journal of Kiswahili · 17.11.2026 · 6 (1) · 188-197

DOI: 10.51317/jbv7vn05 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Editon Consortium Journal of Kiswahili, online erschienen am 17.11.2026. Verfasst von Sumaiya Yunus Mwamzandi und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala haya yanachunguza taswira ya mwanamke katika ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu wa karne ya ishirini na moja kwa kurejelea shairi la Mahavule na Jamii lililoandikwa na Mahmoud Ahmed Abdulkadir. Madhumuni ya makala haya ni kubaini taswira mbalimbali za mwanamke katika miktadha ya kidini, kifamilia, kijamii na kiteknolojia, pamoja na namna usawiri huo unavyodhihirisha mwingiliano kati ya misingi ya Kiisilamu na mabadiliko ya jamii ya kisasa. Utafiti huu ulifanyika nyanjani na ulichukua muundo wa kimaelezo. Mtafiti alitumia usampulishaji wa kimakusudi kupata mtunzi na mashairi ya Kiswahili ya Kiisilamu. Kupitia mbinu ya mahojiano, mtafiti aliweza kupata idadi ya mashairi matano, Mahavule na Jamii likiwa mojawapo. Uchambuzi umeongozwa na nadharia ya Ufeministi wa Kiisilamu na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo yalibainisha kuwa taswira ya mwanamke katika mashairi ya Kiswahili ya Kiisilamu inaendelea kuwa changamano huku mvutano kati ya mafundisho ya Kiisilamu, matarajio ya kitamaduni na mabadiliko ya kijamii na kiteknolojia vikionekana kuwa nguzo kuu za kumjenga/kumdidimiza mwanamke katika jamii ya kisasa.Makala yanahitimisha kuwa shairi la Mahavule na Jamii linajenga taswira ya mwanamke inayojaribu kuoanisha heshima na utambulisho wa kidini na mahitaji ya ushiriki wake katika jamii ya kisasa. Mwanamke anapewa nafasi kubwa katika jamii na maendeleo yanayotegemea pakubwa uwajibikaji wake. Makala hii inatoa mchango muhimu katika fasihi hasa ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu kwa kudhihirisha jinsi dini, utamaduni na mabadiliko ya kiwakati vinaweza kutumiwa na watunzi kwa pamoja kumjenga mwanamke na kuijenga nafasi yake katika jamii ya sasa.

Zitieren

APA

Mwamzandi, S. Y., Kandagor, M., & Wafula, M. (2026). Taswira ya Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu wa Karne ya 21: Uchambuzi wa Shairi la Mahavule na Jamii. Editon Consortium Journal of Kiswahili, 6(1), 188-197. https://doi.org/10.51317/jbv7vn05

Vancouver

Mwamzandi SY, Kandagor M, Wafula M. Taswira ya Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu wa Karne ya 21: Uchambuzi wa Shairi la Mahavule na Jamii. Editon Consortium Journal of Kiswahili. 2026;6(1):188-197. doi:10.51317/jbv7vn05

BibTeX
@article{Mwamzandi2026,
  author = {Mwamzandi, Sumaiya Yunus and Kandagor, Mosol and Wafula, Magdaline},
  title = {Taswira ya Mwanamke katika Ushairi wa Kiswahili wa Kiisilamu wa Karne ya 21: Uchambuzi wa Shairi la Mahavule na Jamii},
  journal = {Editon Consortium Journal of Kiswahili},
  year = {2026},
  volume = {6},
  number = {1},
  pages = {188--197},
  doi = {10.51317/jbv7vn05}
}
Kostenlos starten →