Athari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama
East African Journal of Swahili Studies · 16.11.2026 · 9 (3) · 428-440
DOI: 10.37284/jammk.9.3.6290 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 16.11.2026. Verfasst von Siwema Ally Makunga und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Makala hii imefafanua athari za ujumi wa Kiafrika katika ujenzi wa wahusika wa kike katika tamthiliya ya Nguzo Mama ya Penina Muhando. Lengo lilikuwa kubainisha namna vipengele vya ujumi wa Kiafrika vinavyoathiri utambulisho nafasi, sauti, uwezo, mahusiano na taswira za wahusika wa kike. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Ujumi wa Kiafrika, inayosisitiza uhusiano wa sanaa na maisha, maadili, mazingira, ushirikiano na tajiriba za jamii. Utafiti ulitumia mkabala wa kitaamuli na usanifu wa kifani. Data zilikusanywa kupitia usomaji makini wa tamthiliya iliyoteuliwa, usaili na majadiliano ya vikundi. Washiriki walikuwa 15, wakiwamo wahadhiri watatu wa fasihi ya Kiswahili na wanafunzi 12 waliokuwa na maarifa kuhusu tamthiliya hiyo. Washiriki waliteuliwa kwa usampulishaji lengwa na data zilichambuliwa kwa mkabala wa kimaudhui. Matokeo yanaonesha kuwa ujumi wa Kiafrika una athari chanya na hasi katika ujenzi wa wahusika wa kike. Kwa upande wa athari chanya, matumizi ya usimulizi, nyimbo, ngoma, maleba, majibizano, matendo na taashira yanawatofautisha wahusika kiutambulisho; yanamweka mwanamke katikati ya simulizi; na yanamjenga kama mzalishaji, mlezi, kiongozi, mwenye maarifa na mtetezi wa haki. Vipengele hivyo pia vinadhihirisha uwezo wa wanawake kushirikiana na kushiriki katika maendeleo ya jamii. Kwa upande wa athari hasi, vinamjenga mwanamke kama mhusika anayebebeshwa majukumu mazito ya kifamilia, anayenyanyaswa na mfumo dume, anayetazamwa kupitia mwili, anayekwamishwa na migogoro baina ya wanawake na anayenyimwa nafasi ya kutumia maarifa yake. Kushindwa kuisimamisha Nguzo Mama kunajenga taswira ya ukombozi wa mwanamke ambao haujakamilika. Makala inahitimisha kuwa ujumi wa Kiafrika katika Nguzo Mama si pambo la kisanaa pekee, bali ni nyenzo inayounda wahusika wa kike wenye uwezo, udhaifu na tajiriba zinazofichua migongano ya kijinsia, kiuchumi na kiuongozi katika jamii. Hivyo, wahakiki wa fasihi wanapaswa kutenganisha vipengele vya ujumi, sababu za matumizi yake na athari zake katika ujenzi wa wahusika.
Zitieren
APA
Makunga, S. A., Abdallah, H. K., & Bakari, J. (2026). Athari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 428-440. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6290
Vancouver
Makunga SA, Abdallah HK, Bakari J. Athari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):428-440. doi:10.37284/jammk.9.3.6290
BibTeX
@article{Makunga2026,
author = {Makunga, Siwema Ally and Abdallah, Hadija Kutwa and Bakari, Juma},
title = {Athari za Ujumi wa Kiafrika katika Ujenzi wa Mhusika wa Kike katika Tamthiliya ya Nguzo Mama},
journal = {East African Journal of Swahili Studies},
year = {2026},
volume = {9},
number = {3},
pages = {428--440},
doi = {10.37284/jammk.9.3.6290}
}
EUVIMED