EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi

Harrison Onyango Ogutu, Dr. Sheila Wandera, Prof. Wendo Nabea

Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK) · 2022

DOI: 10.51317/eajk.v2i1.99 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 2022. Verfasst von Harrison Onyango Ogutu und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Watu wenye uwezo na mamlaka wanatumia madaraka yao kuwatawala wengine kwa vishawishianuwai. Asasi za kijamii kama vile ndoa, shule, vyuo, utamaduni na malezi zinaendelea kushuhudiautawala wa wenye uwezo juu ya wasio na uwezo. Licha ya ubayana wa hali hii katika jamii, watafiti na wahakiki wa tanzu za fasihi andishi hususan riwaya hawajaonyesha namna hejemonia inajitokeza katika asasi za kijamii. Ingawa wahakiki wengi wa riwaya wameweza kuangazia masualaya kila nui kuhusu asasi za kijamii, suala la hejemonia katika taasisi hizo lilihitaji kumulikwa. Hivyo,utafiti huu ulidhamiria kuchunguza ujitokezaji wa hejemonia katika safu ya hejemonia ya jamii kwa mujibu wa riwaya za Msimu wa Vipepeo, Dharau ya Ini, Msururu wa Usaliti na Majilio ya Mkombozi.Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya hejemonia ilioasisiwa na Antonio Gramsci katika makala aliyoyaandika akiwa gerezani kati ya mwaka wa 1923 na 1936. Nadharia hii inaelezea udumishaji wauwezo na mamlaka ya tabaka moja kuu juu ya tabaka dogo kwa kutumia mikakati anuwai. Utafitihuu ulifanyiwa maktabani ambako utaratibu wa upekuzi wa yaliyomo ulitumika kukusanya data huku mbinu ya kithamano ikitumika kuchanganua data hiyo. Matokeo ya utafiti huu yatawafaa wahakiki na watafiti wa lugha na fasihi huku yakiweka wazi uwepo wa hejemonia katika asasi za jamii.

Zitieren

APA

Ogutu, H. O., Wandera, D. S., & Nabea, P. W. (2022). Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). https://doi.org/10.51317/eajk.v2i1.99

Vancouver

Ogutu HO, Wandera DS, Nabea PW. Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). 2022. doi:10.51317/eajk.v2i1.99

BibTeX
@article{Ogutu2022,
  author = {Ogutu, Harrison Onyango and Wandera, Dr. Sheila and Nabea, Prof. Wendo},
  title = {Ujitokezaji wa Hejemonia Katika Asasi Za Kijamii: Mfano wa Dharau ya Ini, Msimu wa Vipepeo, Msururu wa Usaliti naMajilio ya Mkombozi},
  journal = {Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)},
  year = {2022},
  doi = {10.51317/eajk.v2i1.99}
}
Kostenlos starten →