Itikadi na Uwezo wa Kijinsia katika Nyimbo za Taarab
Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK) · 2022
DOI: 10.51317/eajk.v2i1.97 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 2022. Verfasst von Mary M. Malenya und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Makala haya yalilenga kuchunguza itikadi inavyomsawiri mwanamke huku ikimpokonya uwezo wa kutekeleza majukumu sawa na mwanamume. Itikadi ndio huwaongoza watu namna wanavyotumia lugha na hivyo kudhihirisha mahusiano ya mamlaka. Usemi huu unadhibitisha hoja zinazowaongoza watunzi wa fasihi hivi kwamba lugha wanayotumia ndio hubainisha nafasi anayopewa mwanajamii. Suala hili liliwezeshwa kwa kuwepo na malengo mawili. Moja, kuchunguza utunzi na maudhui tawala katika nyimbo teule za taarab ili kubaini mafungamano ya masuala hayo na itikadi inayotawala. Pili, kuonyesha mahusiano ya uwezo kati ya mwanamke na mwanamume katika jamii kupitia nyimbo za taarab. Malengo haya yaliafikiwa kupitia uchanganuzi wa matumizi ya lugha katika nyimbo mbili teule za taarab ili kuonyesha usawiri wa mwanamke kwa kuzingatia itikadi na uwezo wa kijinsia. Nyimbo zilizochanganuliwa ni Daktari wa Mapenzi na VIP ambazo zimeimbwa na Mzee Yusuf akiwa na bendi ya Jahazi Modern Taarab nchini Tanzania.Vigezo vikuu vya uteuzi wa nyimbo hizi ni maudhui na lugha. Nadharia zilizotumika ni ufeministi wa Kiafrika inayorejelea masuala ya jinsia ya kike pamoja na Uchanganuzi Hakiki Usemi (UHU) itakayochunguzamatumizi ya lugha. Data za makala haya zilikusanywa kwa kuchanganua nyimbo teule. Mtafiti alisikiza kanda ili kupata matini za kumfaa katika ukusanyaji data. Data iliyokusanywa ilifanyiwa unukuzi, kuainishwa,kupangwa, kuchanganuliwa na kufasiriwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia mbili zilizotumika katika utafiti huu. Data hiyo iliwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Zitieren
APA
Malenya, M. M., Simwa, S. P. W., & Ogola, J. O. (2022). Itikadi na Uwezo wa Kijinsia katika Nyimbo za Taarab. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). https://doi.org/10.51317/eajk.v2i1.97
Vancouver
Malenya MM, Simwa SPW, Ogola JO. Itikadi na Uwezo wa Kijinsia katika Nyimbo za Taarab. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). 2022. doi:10.51317/eajk.v2i1.97
BibTeX
@article{Malenya2022,
author = {Malenya, Mary M. and Simwa, Sheila Pamela Wandera and Ogola, James O.},
title = {Itikadi na Uwezo wa Kijinsia katika Nyimbo za Taarab},
journal = {Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)},
year = {2022},
doi = {10.51317/eajk.v2i1.97}
}
EUVIMED