EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY-NC-SA 4.0

Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil

Jane Jepkoech Singoe, Mwanakombo Mohamed, Mosol Kandagor

Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK) · 2022

DOI: 10.51317/eajk.v2i1.103 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 2022. Verfasst von Jane Jepkoech Singoe und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza jinsi vipengele vya kitamaduni katika matini teule ya Kiswahili na Kikalenjin vilivyochangia mtafsiri kuiandika upya Bukuit ne Tilil. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili, ambazo ni nadharia ya tafsiri vitendo ambayo ilitumika kubaini jinsi tofauti za kimazingira kati ya hadhira ya matini asilia na ya matini pokezi ilivyopelekea uandishi upya kufanyika wakati wa kutafsiri. Nadharia ya pili ni ya ulinganifu,ambapo matini asilia ililinganishwa na matini pokezi ili kubai ni kama ujumbe ulihifadhiwa katika matini tafsiri.Aidha, tamaduni, matumizi ya msamiati na sarufi zililinganishwa kwa kuchunguza mikakati na mbinu zilizotumika kutafsiri matini asilia, na hivyo kubaini uandishi upya katika matini pokezi. Data zilikusanywa kupitia uchunguzi maktabani na vilevile kuwasaili washikadau katika Ofisi ya Utafsiri wa Bibilia ya Kapsabet na Shirika la Kutafsiri Biblia nchini, pamoja na wazungumza lugha ya Kikalenjin ambao walituelekeza juu ya matumizi ya baadhi ya maneno. Usampuli wa kimakusudi ulitumiwa ili kupata data iliyotumika katika uchanganuzi. Kitabu cha Mithali katika Agano la Kale kiliteuliwa kwa minajili ya utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalikuwa: utamaduni wa Waswahili na wa Wakalenjin ni tofauti na hii ilipelekea uandishi upya ufanywe katika tafsiri. Utafiti unapendekeza yafuatayo: Sera za elimu kuhusu lugha za kienyeji zinafaa kutilia maanani tafsiri ya matini za kufundishia.

Zitieren

APA

Singoe, J. J., Mohamed, M., & Kandagor, M. (2022). Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). https://doi.org/10.51317/eajk.v2i1.103

Vancouver

Singoe JJ, Mohamed M, Kandagor M. Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). 2022. doi:10.51317/eajk.v2i1.103

BibTeX
@article{Singoe2022,
  author = {Singoe, Jane Jepkoech and Mohamed, Mwanakombo and Kandagor, Mosol},
  title = {Jinsi Vipengele vya Kitamaduni katika Matini Teule ya Kiswahili na Kikalenjin Vilivyochangia Mtafsiri Kuiandika Upya Bukuit Ne Tilil},
  journal = {Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)},
  year = {2022},
  doi = {10.51317/eajk.v2i1.103}
}
Kostenlos starten →