EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Aina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya

Muiga Harrison Gatuthu, Jackline Murimi, Jacktone Onyango

East African Journal of Swahili Studies · 16.11.2026 · 9 (3) · 462-471

DOI: 10.37284/jammk.9.3.6299 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 16.11.2026. Verfasst von Muiga Harrison Gatuthu und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Katika utoaji wa huduma za afya, lugha ni nyenzo muhimu inayowezesha mawasiliano bora kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa. Mawasiliano yenye ufanisi husaidia katika utoaji wa taarifa sahihi, uelewa wa maelekezo ya kitabibu na kuboresha ubora wa huduma za afya. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa lugha inayotumika katika mazingira ya afya huathiri namna taarifa zinavyowasilishwa, kueleweka na kutekelezwa na wagonjwa. Utafiti huu ulichunguza aina za lugha zinazotumika katika mawasiliano kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa katika Hospitali Kuu ya Thika. Pia ulilenga kubaini sababu zinazoathiri matumizi ya lugha, changamoto zinazojitokeza na athari za lugha katika uelewa wa wagonjwa. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Sajili na Nadharia ya Umitindo. Nadharia ya Sajili inaeleza kuwa matumizi ya lugha hutegemea muktadha wa mawasiliano, mazingira na mahitaji ya washiriki. Nadharia ya Umitindo inaonyesha kuwa wazungumzaji hubadili mtindo wa lugha kulingana na hali, hadhira na madhumuni ya mawasiliano. Nadharia hizi zilisaidia kueleza namna wataalamu wa afya huchagua lugha wanapowasiliana na wagonjwa. Utafiti ulitumia muundo wa mbinu mseto uliounganisha mbinu za kiasi na ubora. Data zilikusanywa kwa kutumia hojaji na mahojiano kutoka kwa wagonjwa na wataalamu wa afya katika Hospitali Kuu ya Thika. Sampuli ilijumuisha wagonjwa arobaini (40) na wataalamu wa afya watano (5) walioteuliwa kwa kutumia usampulishaji nasibu. Uhalali wa vifaa vya utafiti ulithibitishwa kwa kutumia Cronbach Alpha, ambapo kiwango cha 0.82 kilionyesha utegemezi wa vifaa hivyo.Data zilichanganuliwa kwa kutumia SPSS kwa data za kiasi na uchanganuzi wa mada kwa data za ubora. Matokeo yalionyesha kuwa Kiswahili ndicho lugha iliyotumika zaidi katika mawasiliano kati ya wataalamu wa afya na wagonjwa, kikifuatiwa na Kiingereza na lugha za kienyeji. Utafiti ulibaini kuwa matumizi ya lugha rahisi huongeza uelewa wa wagonjwa, ilhali istilahi ngumu za kitabibu na tofauti za lugha husababisha changamoto. Utafiti unapendekeza matumizi ya lugha rahisi, mafunzo ya mawasiliano kwa wataalamu wa afya, matumizi ya wakalimani na tafiti zaidi kuhusu matumizi ya lugha katika hospitali nyingine nchini Kenya.

Zitieren

APA

Gatuthu, M. H., Murimi, J., & Onyango, J. (2026). Aina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 462-471. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6299

Vancouver

Gatuthu MH, Murimi J, Onyango J. Aina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):462-471. doi:10.37284/jammk.9.3.6299

BibTeX
@article{Gatuthu2026,
  author = {Gatuthu, Muiga Harrison and Murimi, Jackline and Onyango, Jacktone},
  title = {Aina za Lugha Zinazotumika katika Mawasiliano Kati ya Wataalamu wa Lishe na Wagonjwa: Utafiti wa Hospitali Kuu ya Thika, Kenya},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {3},
  pages = {462--471},
  doi = {10.37284/jammk.9.3.6299}
}
Kostenlos starten →