Misemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda
East African Journal of Swahili Studies · 16.11.2026 · 9 (3) · 441-461
DOI: 10.37284/jammk.9.3.6291 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 16.11.2026. Verfasst von Picton Kansiime und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mchango wa misemo ya kidini iliyopo kwenye magari mpaka wa Mutukula wilayani Kyotera katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili miongoni mwa wananchi. Malengo mahususi ya utafiti huu ni kuchambua misemo ya kidini inayopatikana kwenye magari katika matumizi ya Kiswahili pamoja na athari zake katika maadili ya kijamii na mawasiliano ya kila siku. Utafiti huu ulitumia muundo wa kimaelezo. Data zilikusanywa kupitia mbinu za uchunguzi wa moja kwa moja, dodoso, na mahojiano. Walengwa wa utafiti walikuwa madereva wa magari ya usafiri wa umma, wamiliki wa magari, abiria na wakazi wa eneo la mpakani pamoja na viongozi wa dini. Sampuli ya jumla ya washiriki 25 ilitumika, na walichaguliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa usampulishaji. Data za kimaelezo zilichambuliwa kwa kutumia mbinu ya uchambuzi wa mada, ilhali data za kiasi zilichambuliwa kwa kutumia asilimia na takwimu rahisi. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa misemo ya kidini kwenye magari ina mchango mkubwa katika kukuza matumizi ya Kiswahili. Ilibainika kuwa misemo hiyo inatumika kama njia ya mawasiliano ya kijamii, ilipanua msamiati wa Kiswahili, na kuimarisha matumizi ya lugha fasaha miongoni mwa wananchi. Misemo hiyo inasaidia kuhamasisha maadili mema kama vile upendo, amani, uvumilivu na heshima katika jamii ya mpakani. Utafiti ulipendekeza kuwa misemo hiyo iandaliwe kwa Kiswahili sanifu, ihusishe wataalamu wa lugha na viongozi wa dini, na itumike kama nyenzo ya kufundishia na kukuza Kiswahili katika jamii. Aidha, serikali na taasisi za lugha zilihimizwa kuunga mkono matumizi ya maandishi ya umma yenye ubora ili kuimarisha lugha na maadili ya kijamii. Kwa ujumla, utafiti ulihitimisha kuwa misemo ya kidini kwenye magari ni nyenzo muhimu ya kijamii na kiisimu inayochangia kwa kiasi kikubwa kukuza Kiswahili, kuimarisha mawasiliano na kudumisha maadili katika jamii ya mpakani Mutukula.
Zitieren
APA
Kansiime, P., Atukunda, E., & Kanwa, O. (2026). Misemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 441-461. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6291
Vancouver
Kansiime P, Atukunda E, Kanwa O. Misemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):441-461. doi:10.37284/jammk.9.3.6291
BibTeX
@article{Kansiime2026,
author = {Kansiime, Picton and Atukunda, Edwine and Kanwa, Olivia},
title = {Misemo ya Kidini Iliyopo kwenye Magari na Ukuzaji wa Kiswahili Mpakani Mutukula Wilayani Kyotera, Uganda},
journal = {East African Journal of Swahili Studies},
year = {2026},
volume = {9},
number = {3},
pages = {441--461},
doi = {10.37284/jammk.9.3.6291}
}
EUVIMED