EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Changamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Maumbo ya Ukanushi: Mfano wa Wanafunzi wa Shule Teule za Upili Gatsibo, Rwanda

Appolinaire Nshimiyimana, Wallace Kapele Mlaga, Laurien Tuyishimire

East African Journal of Swahili Studies · 21.07.2026 · 9 (2) · 41-54

DOI: 10.37284/jammk.9.2.5394 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 21.07.2026. Verfasst von Appolinaire Nshimiyimana und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala hii inajadili changamoto za ufundishaji na ujifunzaji wa maumbo ya ukanushi miongoni mwa wanafunzi wa shule za upili nchini Rwanda. Makala yetu yanaongozwa na malengo mahususi mawili: Mosi ni kuchunguza changamoto za ubainishaji wa maumbo ya ukanushi. Pili ni kuunda mikakati ya kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji wa maumbo ya ukanushi. Data za makala zilikusanywa kupitia uchambuzi wa nyaraka, ushuhudiaji na mahojiano. Data za makala zilichambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya Isimu Msingi iliyoasisiwa na Dixon (1997). Matokeo ya utafiti yalionesha kwamba walimu wa Kiswahili wana mitazamo tofauti juu ya maumbo ya ukanushi na wanayafundisha namna tofauti kulingana na mitazamo waliyonayo. Kutokana na hayo, wanafunzi hawayafahamu maumbo ya ukanushi na hawawezi kuyatumia maumbo yote kutunga sentensi sahihi katika Kiswahili. Hivyo basi, utafiti ulibainisha mikakati ya kuboresha na kufanikisha ufundishaji na ujifunzaji wa ukanushi. Mkakati wa kwanza ni pamoja na kuwapa wanafunzi mazoezi ya kuyalinganisha maumbo ya ukanushi. Mkakati wa pili ni kuwapatia wanafunzi mazoezi ya kubadilisha sentensi kwa kuzingatia mofu. Mkakati wa tatu ni ushirikiano miongoni mwa walimu kwa ajili ya kukuza umahiri wao. Hivyo basi, makala haya yanapendekeza mafunzo ya walimu juu ya ufundishaji wa maumbo ya ukanushi.

Zitieren

APA

Nshimiyimana, A., Mlaga, W. K., & Tuyishimire, L. (2026). Changamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Maumbo ya Ukanushi: Mfano wa Wanafunzi wa Shule Teule za Upili Gatsibo, Rwanda. East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 41-54. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5394

Vancouver

Nshimiyimana A, Mlaga WK, Tuyishimire L. Changamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Maumbo ya Ukanushi: Mfano wa Wanafunzi wa Shule Teule za Upili Gatsibo, Rwanda. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):41-54. doi:10.37284/jammk.9.2.5394

BibTeX
@article{Nshimiyimana2026,
  author = {Nshimiyimana, Appolinaire and Mlaga, Wallace Kapele and Tuyishimire, Laurien},
  title = {Changamoto za Ufundishaji na Ujifunzaji wa Maumbo ya Ukanushi: Mfano wa Wanafunzi wa Shule Teule za Upili Gatsibo, Rwanda},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {2},
  pages = {41--54},
  doi = {10.37284/jammk.9.2.5394}
}
Kostenlos starten →