EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Mchango wa Kinaya cha Usemi katika Ukuzaji wa Stadi za Utambuzi, Hisia na Kijamii kwa Watoto

Agatha Marigu Njeru, John Khaisie Wanyama, Allan Mugambi

East African Journal of Swahili Studies · 09.07.2026 · 9 (2) · 13-27

DOI: 10.37284/jammk.9.2.5313 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 09.07.2026. Verfasst von Agatha Marigu Njeru und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala haya yanachunguza manufaa ya kinaya cha usemi katika mawasiliano kati ya mzazi na watoto katika jamii, kwa njia ya kithamano. Usamplishaji wa kimaksudi ulitumiwa ili kuteua washiriki katika utafiti pamoja na data ya uchanganuzi. Data zilikusanywa kupitia mbinu ya mijadala ya makundi zingativu sita yaliyoshirikisha vijana ishirini na moja (21) ambao walikumbuka uzoefu wa utotoni kuhusu matumizi ya kinaya cha usemi, na wazazi ishirini (20) wakijadili mikakati yao ya kimawasiliano ya kinaya ndani ya familia, katika eneo la Embu, kaunti dogo la Embu Magharibi. Data ilichanganuliwa kimaudhui kwa kuegemea mtazamo unaotolewa na Nadharia ya Kisingizio-Dokezo na Kujifanya. Matokeo yalifichua kuwa matumizi ya mara kwa mara ya kinaya cha usemi humwezesha mtoto katika ukuzaji wa stadi ya utambuzi kwani anahitajika kutambua maana zinazokusudiwa. Pia, husababisha udhibiti wa hisia na utatuzi wa migogoro ya watoto wanapokabiliwa na uchakataji wa hisia zinazojitokeza wakati wa matumizi yake. Kinaya cha usemi huimarisha lugha na utamaduni, kwani ufichuzi wake unachukuliwa kuwa na uwezo wa kudumisha maadili katika jamii. Utafiti huu unachangia uelewa wa lugha katika jamii na malezi kwa kuonyesha dhima muhimu ya kinaya katika mawasiliano. Mchango huu unanuia kuboresha uwezo wa kipragmatiki, kijamii na kiutambuzi wa watoto.

Zitieren

APA

Njeru, A. M., Wanyama, J. K., & Mugambi, A. (2026). Mchango wa Kinaya cha Usemi katika Ukuzaji wa Stadi za Utambuzi, Hisia na Kijamii kwa Watoto. East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 13-27. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5313

Vancouver

Njeru AM, Wanyama JK, Mugambi A. Mchango wa Kinaya cha Usemi katika Ukuzaji wa Stadi za Utambuzi, Hisia na Kijamii kwa Watoto. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):13-27. doi:10.37284/jammk.9.2.5313

BibTeX
@article{Njeru2026,
  author = {Njeru, Agatha Marigu and Wanyama, John Khaisie and Mugambi, Allan},
  title = {Mchango wa Kinaya cha Usemi katika Ukuzaji wa Stadi za Utambuzi, Hisia na Kijamii kwa Watoto},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {2},
  pages = {13--27},
  doi = {10.37284/jammk.9.2.5313}
}
Kostenlos starten →