SEMANTIKI YA MAJINA YA WALUO NCHINI KENYA
International Research Journal of Rongo University · 02.11.2026 · 4 (2) · 86-94
DOI: 10.64535/ijoru.v4i2.151 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift International Research Journal of Rongo University, online erschienen am 02.11.2026. Verfasst von Jael Akinyi Owala und 2 weiteren Autor:innen. Die Arbeit nennt 16 Literaturangaben. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-ND 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Majina ya watu katika jamii za Kiafrika hubeba maana zinazohusiana na utamaduni, historia na mazingira ya kijamii. Miongoni mwa Waluo wa Kenya, majina si alama za utambulisho pekee, bali pia huakisi mitazamo ya jamii kuhusu maisha na matukio yanayohusiana na kuzaliwa kwa mtoto. Ingawa tafiti mbalimbali zimechunguza majina ya Kiafrika kwa mitazamo tofauti ya kiisimu, tafiti chache zimejikita katika kuchanganua maana za majina ya Waluo kwa mtazamo wa kisemantiki. Makala hii inalenga kuchunguza ruwaza za kisemantiki katika majina ya watu miongoni mwa Waluo nchini Kenya ili kubainisha maana zinazojitokeza katika majina hayo. Data ilikusanywa kutoka orodha za majina katika afisi za usajili wa watoto katika Kaunti ya Migori, mahojiano ya wazungumzaji wa Dholuo, pamoja na maandishi kuhusu majina ya Kiafrika. Data zilichanganuliwa kwa kutumia Nadharia ya Ujinaishaji ya Mill (1970). Matokeo yanaonyesha kuwa majina ya Waluo huakisi matukio ya kuzaliwa, hali za kijamii, imani za kitamaduni na matarajio ya wazazi. Maana zilizobainika ni pamoja na maana za kihusishi, dhamirifu, kijamii na dhanishi. Makala hii inahitimisha kuwa majina ya Waluo huonesha uhusiano kati ya lugha, utamaduni na mawasiliano, na pia huhifadhi utambulisho na urithi wa kiutamaduni.
Zitieren
APA
Owala, J. A., Nyandiba, C., & Ontieri, J. (2026). SEMANTIKI YA MAJINA YA WALUO NCHINI KENYA. International Research Journal of Rongo University, 4(2), 86-94. https://doi.org/10.64535/ijoru.v4i2.151
Vancouver
Owala JA, Nyandiba C, Ontieri J. SEMANTIKI YA MAJINA YA WALUO NCHINI KENYA. International Research Journal of Rongo University. 2026;4(2):86-94. doi:10.64535/ijoru.v4i2.151
BibTeX
@article{Owala2026,
author = {Owala, Jael Akinyi and Nyandiba, Carren and Ontieri, James},
title = {SEMANTIKI YA MAJINA YA WALUO NCHINI KENYA},
journal = {International Research Journal of Rongo University},
year = {2026},
volume = {4},
number = {2},
pages = {86--94},
doi = {10.64535/ijoru.v4i2.151}
}
EUVIMED