Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo
Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK) · 2022
DOI: 10.51317/eajk.v2i1.108 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK), 2022. Verfasst von Nyongesa Salyne und 2 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY-NC-SA 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Utafiti huu unachunguza mikondo mipya katika mashairi yanayochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, kumbi ya Ushairi Wenu na Sokomoko, katika kipindi cha Januari 1, 2018 hadi Agosti 31, 2019. Utafiti uliongozwa na nadharia ya kimtindo ya Leech na Short (2007) ili kuafikia lengo letu. Mihimili mitatu ya nadharia hii ilitumiwa ili kufanikisha lengo la mtafiti, nayo ni: Fasihi ni muundo wa lugha na kwa hivyo lazima matumizi ya lugha yazingatiwe, uhakiki wa kifasihi haupaswi kupuuza matumizi ya vipengele vya isimu lugha ikiwemo. Data iliyotumiwa katika utafiti ilikusanywa maktabani na mitandaoni kupitia usomaji wa tasnifu, vitabu, majarida na magazeti. Uteuzi sampuli wa kimakusudi ulitumiwa kuteua mashairi yaliyosheheni upya katika mikondo.Uchanganuzi na uwasilishaji wa data ulifanywa kupitia kwa maelezo.Matokeo ya utafiti yalionyesha kwamba,mashairi ya ushairi wenu na sokomoko yanasheheni mikondo mipya ya utunzi ikiwemo: Matumizi ya Sheng’,usimulizi na kuwepo kwa mianzo ya kifomula. Mashairi yaliyotumika yalitolewa katika kumbi za Sokomoko na Ushairi Wenu ambazo ni kumbi zinazochapisha mashairi ya watunzi mbalimbali katika gazeti la Taifa Leo.Matokeo ya utafiti yalionesha namna mikondo mipya ya utunzi inaendelea kuibuliwa na watunzi wa mashairi kila uchao. Mashairi yaliyotumika hapa hata hivyo, ni yale ya kiarudhi pekee kwani ndiyo yachapishwayo katika gazeti la Taifa Leo.Makala haya yatakuwa ya manufaa kwa walimu wa Kiswahili, wanafunzi na watafiti wengine wanaotafitia suala la upya katika utunzi wa mashairi.
Zitieren
APA
Salyne, N., Simwa, S. W., & Nabea, W. (2022). Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). https://doi.org/10.51317/eajk.v2i1.108
Vancouver
Salyne N, Simwa SW, Nabea W. Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo. Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK). 2022. doi:10.51317/eajk.v2i1.108
BibTeX
@article{Salyne2022,
author = {Salyne, Nyongesa and Simwa, Sheila Wandera- and Nabea, Wendo},
title = {Mikondo Mipya katika Utunzi wa Mashairi: Mifano Kutoka ‘Sokomoko’na ‘UshairiWenu’Katika Gazeti la Taifa Leo},
journal = {Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)},
year = {2022},
doi = {10.51317/eajk.v2i1.108}
}
EUVIMED