EUVIMEDEUVIMED entdecken
Crossref

Uhalisia wa Maudhui ya Usalama katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Kijana Mpelelezi,Wamitila K.W (2007) Na Usiku wa Manane,Kobia J. (2010)

ROSE NDANU MBOYA

European Journal of Linguistics · 2022

DOI: 10.47941/ejl.1001 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift European Journal of Linguistics, 2022. Verfasst von ROSE NDANU MBOYA.

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala hii inachunguza uhalisia wa maudhui ya usalama katika fasihi ya watoto kwa kuchanganua riwaya ya Kijana Mpelelezi (Wamitila, 2007) na Usiku wa Manane (Kobia, 2010). Hadithi hizi za watoto zimejikita katika fasihi ya watoto. Madhumuni ya utafiti huu ni kubainisha masuala ya usalama yaliyodhihirishwa na waandishi wa riwaya za Usiku wa Manane (Kobia, 2010) na Kijana Mpelelezi (Wamitila, 2007), kueleza jinsi wahusika watoto wanaohusishwa na maudhui ya usalama wanavyosawiriwa na kutathmini uhalisia wa maudhui yanayohusu usalama na yanayonuiwa watoto kama hadhira lengwa katika riwaya za Usiku wa Manane (Kobia, 2010) na Kijana Mpelelezi (Wamitila, 2007). Nadharia za uhalisia wa kijamaa na Soshiolojia ya fasihi zilitoa msingi madhubuti kuhusu mada husika. Makala hii inathibitisha kuwa masuala ya usalama yanayobainika yanafungamana na hali ilivyo katika maisha ya jamii ya karne hii ya ishirini na moja. Vita vya kikabila na ukosefu wa usalama katika jamii vinapaswa kuondolewa na kusahaulika kabisa. Hadithi za watoto za waandishi hawa zinadhihirisha uhalisia wa maudhui ya usalama. Ni dhahiri kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za dharura kuwafahamisha watoto kuhusu umuhimu wa amani katika taifa ili wakikua wawe na uwezo wa kueneza maridhiano baina ya jamii lugha zote.

Zitieren

APA

MBOYA, R. N. (2022). Uhalisia wa Maudhui ya Usalama katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Kijana Mpelelezi,Wamitila K.W (2007) Na Usiku wa Manane,Kobia J. (2010). European Journal of Linguistics. https://doi.org/10.47941/ejl.1001

Vancouver

MBOYA RN. Uhalisia wa Maudhui ya Usalama katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Kijana Mpelelezi,Wamitila K.W (2007) Na Usiku wa Manane,Kobia J. (2010). European Journal of Linguistics. 2022. doi:10.47941/ejl.1001

BibTeX
@article{MBOYA2022,
  author = {MBOYA, ROSE NDANU},
  title = {Uhalisia wa Maudhui ya Usalama katika Fasihi ya Watoto: Mfano wa Riwaya ya Kijana Mpelelezi,Wamitila K.W (2007) Na Usiku wa Manane,Kobia J. (2010)},
  journal = {European Journal of Linguistics},
  year = {2022},
  doi = {10.47941/ejl.1001}
}
Kostenlos starten →