EUVIMEDEUVIMED entdecken
Crossref

Athari za Unyambulishaji katika Uelekezi wa Vitenzi vya Lugha ya Kimasai

Anna Lomayani, Perida Mgecha

Kioo cha Lugha · 2023

DOI: 10.4314/kcl.v21i1.2 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift Kioo cha Lugha, 2023. Verfasst von Anna Lomayani und 1 weiteren Autor:innen.

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Makala hii inachunguza namna unyambulishaji unavyoathiri uelekezi wa vitenzi katika lugha ya Kimasai. Malengo mahususi ya makala hii ni kubainisha aina za uelekezi, kueleza uelekezi unavyojitokeza na kuchambua namna unyambulishaji unavyoathiri uelekezi wa vitenzi katika lugha ya Kimasai. Makala hii imeongozwa na Nadharia ya Uhusika iliyoasisiwa na Noam Chomsky (1981). Watoataarifa wamepatikana kwa mbinu za usampulishaji tajiriba na tajwa. Data za makala hii zimekusanywa kwa mbinu za tafsiri na ukalimani na uchambuzi wa data umefanyika kwa kutumia mbinu ya kusimba maudhui. Matokeo ya makala hii yanaonesha kuwa lugha ya Kimasai ina aina tatu za uelekezi ambazo ni uelekezi wa yambwa moja, wa yambwa mbili na wa yambwa kapa. Aidha, utafiti umebaini kuwa katika lugha ya Kimasai, yambwa hujitokeza baada ya mtenda ambayo ni tofauti na lugha nyingine, kama vile Kiswahili ambapo yambwa hutokea baada ya kitenzi. Kwa upande wa athari za unyambulishaji katika uelekezi wa vitenzi vya lugha ya Kimasai, husababisha kuongezeka, kuhamishwa au kudondoshwa kwa yambwa. Hata hivyo, tafiti zaidi zinazochunguza vipengele vingine vya kiisimu katika lugha ya Kimasai zinahitajika.

Zitieren

APA

Lomayani, A., & Mgecha, P. (2023). Athari za Unyambulishaji katika Uelekezi wa Vitenzi vya Lugha ya Kimasai. Kioo cha Lugha. https://doi.org/10.4314/kcl.v21i1.2

Vancouver

Lomayani A, Mgecha P. Athari za Unyambulishaji katika Uelekezi wa Vitenzi vya Lugha ya Kimasai. Kioo cha Lugha. 2023. doi:10.4314/kcl.v21i1.2

BibTeX
@article{Lomayani2023,
  author = {Lomayani, Anna and Mgecha, Perida},
  title = {Athari za Unyambulishaji katika Uelekezi wa Vitenzi vya Lugha ya Kimasai},
  journal = {Kioo cha Lugha},
  year = {2023},
  doi = {10.4314/kcl.v21i1.2}
}
Kostenlos starten →