Dosari za kisarufi za wanafunzi wanaojifunza Kiswahili sanifu katika vyuo vikuu nchini Burundi
Kioo cha Lugha · 2023
DOI: 10.4314/kcl.v20i2.6 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift Kioo cha Lugha, 2023. Verfasst von Dieudonné Butoyi und 1 weiteren Autor:innen.
Abstract (Originalsprache)
Utafiti huu ulichunguza aina za dosari za kisarufi zinazofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili sanifu kama lugha ya pili katika baadhi ya vyuo vikuu nchini Burundi. Data zilikusanywa kutoka kwa wanafunzi wanaosoma mwaka wa pili na wa tatu katika vyuo vikuu husika. Usampulishaji nasibu ulitumika kupata sampuli ya washiriki 80. Data zilikusanywa kwa njia za hojaji na upitiaji nyaraka. Matokeo yalionesha kuwa wanafunzi hufanya dosari mbalimbali za kisarufi katika makundi makubwa manne ya kisarufi ambayo ni: ya kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia na kisemantiki. Dosari hizi zinazotokana na athari za lugha za awali katika Kiswahili sanifu zilidhihirisha hali ya wanafunzi kutoweza kubainisha tofauti kati ya mifumo ya kisarufi ya lugha hizo za awali na ule wa Kiswahili sanifu.
Zitieren
APA
Butoyi, D., & Elisifa, Z. (2023). Dosari za kisarufi za wanafunzi wanaojifunza Kiswahili sanifu katika vyuo vikuu nchini Burundi. Kioo cha Lugha. https://doi.org/10.4314/kcl.v20i2.6
Vancouver
Butoyi D, Elisifa Z. Dosari za kisarufi za wanafunzi wanaojifunza Kiswahili sanifu katika vyuo vikuu nchini Burundi. Kioo cha Lugha. 2023. doi:10.4314/kcl.v20i2.6
BibTeX
@article{Butoyi2023,
author = {Butoyi, Dieudonné and Elisifa, Zelda},
title = {Dosari za kisarufi za wanafunzi wanaojifunza Kiswahili sanifu katika vyuo vikuu nchini Burundi},
journal = {Kioo cha Lugha},
year = {2023},
doi = {10.4314/kcl.v20i2.6}
}
EUVIMED