Namna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri
East African Journal of Swahili Studies · 17.11.2026 · 9 (3) · 472-484
DOI: 10.37284/jammk.9.3.6306 ↗Kurz gefasst
Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 17.11.2026. Verfasst von Elizabeth Wayua Francis. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).
Abstract (Originalsprache)
Utafiti huu ulichunguza namna mtindo unavyotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha maudhui ya kifo katika riwaya ya Chozi la Heri (2014) ya Assumpta K. Matei. Mtindo ni kipengele muhimu cha kisanaa kinachomwezesha mwandishi kuwasilisha maudhui kwa namna ya kipekee na yenye mvuto kwa wasomaji. Katika kazi za fasihi, maudhui ya kifo yanaweza kuwasilishwa kupitia uteuzi wa lugha na matumizi ya mbinu mbalimbali za kimtindo zinazosaidia kujenga taswira, kuibua hisia na kusisitiza ujumbe unaokusudiwa. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umitindo kwa mujibu wa Leech (2013), iliyowezesha kuchunguza uteuzi wa lugha na mbinu za kisanaa zinazotumiwa na mwandishi katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Muundo wa utafiti uliotumika ni wa kimaelezo. Eneo la utafiti ni fasihi ya Kiswahili, huku sampuli ya utafiti ikiwa riwaya ya Chozi la Heri (2014), iliyoteuliwa kimakusudi kutokana na namna inavyoshughulikia maudhui ya kifo. Data zilikusanywa kupitia usomaji makini wa riwaya teule zaidi ya mara moja na kunakili vifungu vilivyohusiana na matumizi ya mtindo katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Data hizo zilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia mhimili wa nadharia ulioteuliwa. Matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa mwandishi alitumia mbinu mbalimbali za kimtindo zikiwemo tashbihi, tashihisi, methali, nahau na tafsida katika kuwasilisha maudhui ya kifo. Utafiti ulihitimisha kuwa mtindo una nafasi muhimu katika kuwasilisha na kuimarisha maudhui ya kifo katika riwaya ya Chozi la Heri (2014), kwani matumizi ya lugha na mbinu mbalimbali za kisanaa yanamwezesha mwandishi kuibua hisia, kujenga taswira na kufikisha ujumbe kwa ufanisi zaidi. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuwa na manufaa kwa wanafunzi, walimu, wahakiki na wanazuoni wa fasihi ya Kiswahili kwa kupanua maarifa kuhusu mchango wa mtindo katika uwasilishaji wa maudhui ya kifo katika kazi za fasihi.
Zitieren
APA
Francis, E. W. (2026). Namna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri. East African Journal of Swahili Studies, 9(3), 472-484. https://doi.org/10.37284/jammk.9.3.6306
Vancouver
Francis EW. Namna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(3):472-484. doi:10.37284/jammk.9.3.6306
BibTeX
@article{Francis2026,
author = {Francis, Elizabeth Wayua},
title = {Namna Mtindo Unavyotumika na Mwandishi katika Kuwasilisha Maudhui ya Kifo Kwenye Riwaya ya Chozi la Heri},
journal = {East African Journal of Swahili Studies},
year = {2026},
volume = {9},
number = {3},
pages = {472--484},
doi = {10.37284/jammk.9.3.6306}
}
EUVIMED