EUVIMEDEUVIMED entdecken
Open Access · CC BY 4.0

Uchunguzi Wa Dhima Na Mbinu Za Uundaji Wa Majina Ya Watu Yanayotokana Na Semi Za Kinyankole

Loice Natukunda, Adventina Buberwa

East African Journal of Swahili Studies · 28.07.2026 · 9 (2) · 77-91

DOI: 10.37284/jammk.9.2.5435 ↗

Kurz gefasst

Fachartikel in der Zeitschrift East African Journal of Swahili Studies, online erschienen am 28.07.2026. Verfasst von Loice Natukunda und 1 weiteren Autor:innen. Der Volltext ist frei zugänglich (Open Access, CC BY 4.0).

AbstractBibliografische AngabenZitierenVerwandte Studien

Abstract (Originalsprache)

Utafiti huu unahusu uchunguzi wa dhima na mbinu za uundaji wa majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole, kufafanua dhima za majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole na kueleza mbinu za uundaji wa majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya usaili wa ana kwa ana, zimewasilishwa kwa kutumia majedwali na kuchambuliwa kwa kuongozwa na mkabala wa kinadharia wa Uchanganuzi Tunduizi Kilongo. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole yana dhima ambazo zimefungamana na utamaduni wa Wanyankole. Hii inatokana na dhima za majina hayo kudokeza masuala mbalimbali ya kijamii. Utafiti huu umebaini kwamba majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole yanaundwa kwa kutumia mbinu ya kuhamisha maana yaani maana ya semi kuihamishia kwenye jina la mtu. Mbinu hii hutumika sambamba na mbinu zingine kama vile ufupishaji, udondoshaji wa viambishi tangulizi, uambishaji wa viambishi awali na mwambatano. Kulingana na matokeo hayo, utafiti huu unahitimisha kwamba majina mengi ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole yana dhima ambazo zimefungamana na jamii. Aidha, utafiti huu unahitimisha kwamba mbinu za uundaji wa majina ya watu yanayotokana na semi za Kinyankole zinatofautiana na mbinu zingine za uundaji wa majina. Hii ni kwa sababu, jina haliundwi kwa mbinu moja bali huundwa kwa mbinu ambazo zina mwingiliano ambao ni tofauti na mbinu za uundaji wa majina mengine kama vile majina ya mahali na majina ya kibiashara. Licha ya mahitimisho haya, utafiti huu umeacha mwanya wa kufanyika kwa tafiti zingine kuhusiana na majina katika jamii zingine. Hii ni kwa sababu dhima za majina na mbinu za uundaji wa majina yanayotokana na semi ni za kimahususi.

Zitieren

APA

Natukunda, L., & Buberwa, A. (2026). Uchunguzi Wa Dhima Na Mbinu Za Uundaji Wa Majina Ya Watu Yanayotokana Na Semi Za Kinyankole. East African Journal of Swahili Studies, 9(2), 77-91. https://doi.org/10.37284/jammk.9.2.5435

Vancouver

Natukunda L, Buberwa A. Uchunguzi Wa Dhima Na Mbinu Za Uundaji Wa Majina Ya Watu Yanayotokana Na Semi Za Kinyankole. East African Journal of Swahili Studies. 2026;9(2):77-91. doi:10.37284/jammk.9.2.5435

BibTeX
@article{Natukunda2026,
  author = {Natukunda, Loice and Buberwa, Adventina},
  title = {Uchunguzi Wa Dhima Na Mbinu Za Uundaji Wa Majina Ya Watu Yanayotokana Na Semi Za Kinyankole},
  journal = {East African Journal of Swahili Studies},
  year = {2026},
  volume = {9},
  number = {2},
  pages = {77--91},
  doi = {10.37284/jammk.9.2.5435}
}
Kostenlos starten →